Hizi ndio dalili 8 za kuonyesha umependwa na mwanaume lakini anaogopa kukuambia

Tukija maswala ya kutongoza, kuna mitindo tofauti tofauti ambayo wanaume hutumia ili kufaniikisha lengo lao. Kuna ule msemo unaosema ‘mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani, yaani unaweza kufuata njia tofauti tofauti kufika pahali lakini mwishowe utarudi pale pale sehemu moja, kewahiyo  kwa wanaume kila mmoja ana mbinu yake ya kutongoza. Usije kusema kuwa mwanaume mwenye aibu hajui kutongoza akiwa na wewe, labda hio aibu yake ni moja ya mtego aliouweka spesheli wa kukunasa wewe.

Je utajuaje kama mwanaume mwenye aibu amekuzimia lakini hataki kuonyesha?

1. Anaingiwa na wasiwasi akiwa na wewe
Ukiona mwanaume anaingiwa na kibaridi ama kupapatika akiwa kando yako ujue ni ishara ya kukuambia kuwa amekuzimia. Hii inatokea wakati mko pamoja halafu anaingiwa na wasiwasi mara anafanya hivi mara vile.

2. Anapenda kuulizia marafiki zako kukuhusu
Mwanaume mwenye aibu akikupenda huwa anataka kukufahamu zaidi kukuhusu. Iwapo atashindwa kuongea na wewe moja kwa moja basi ataanza kuwaulizia marafiki zake kukuhusu. Ukiona mwanaume ana tabia kama hii ya kuulizia marafiki zako, lile la kufanya nikuonyesha ishara za kuwa uko huru kuongea nayeye wakati wowote ule anapojiskia huru.

3. Anakuwa na tabia isiyoeleweka akikuona
Wakati mwingine inatokea ya kuwa mwanaume mwenye aibu anashindwa kustahamili kuonyesha hisia zake hivyo kujaribu kuzificha ili usiweze kuzitambua. Lakini badala ya kuzificha, huibua tabia nyingine ambazo hazina mfanano wa kwake. Usishtuke ukiona akifanyika mambo ambayo si ya kawaida manake wewe ndio chanzo kikuu cha kufanyika hivyo. Yaani utakuwa umempagawisha kiasi cha kuwa anaweza kuanza kuchora miduara kwa mchanga akitumia miguu yake.

5. Anapenda kutabasamu na wewe
Wanaume wote kawaida wakipendezwa na mwanamke huwa wanatabasamu. Lakini kwa mwanaume mwenye aibu aliyekupenda huwa tabasamu lake ni tofauti. Mara nyingi atakuwa akitabasamu lakini mara kwa mara anashindwa kukuangalia usoni. Labda anaweza kukuangalia lakini pindi utakapomuangalia yeye atajifanya anaagalia kando. Hii ni baadhi ya tabia ya wanaume wa aibu hufanya wakati anapojaribu kukupendeza.

6. Anakuwa kimya ukiwa naye
Anaweza kuwa anaongea na marafiki zake sehemu flani, lakini pindi utakapotokea ananyamaza kabisa ama kuanza kuongea maneno yasiyoeleweka. Hata usishangae iwapo atakataa kujibu salam zako kama umempata katika hali kama hii. Mara nyingi ukimkuta akiwa na maongezi na marafiki zake, atajifanya hata hakuwa akizungumza katika kuchangia maongezi.

7. Anabadilisha mwonekano wake
Ukiona kuwa mwanaume mwenye aibu ameanza kubadilisha mionekano yake kwa kuanza kuvalia nguo tofauti, mitindo mipya ya nywele nk akiwa na wewe, jua hii ni ishara ya haraka kuonyesha kuwa amekuzimia.  Kufanya hivi kwa kawaida ana makusudio ya kukuridhisha wewe. Labda anadhania ya kuwa kuna mtindo fulani ambao akiuvaa unakupendeza.

8. Anagugumiza akiongea na wewe
Mwanaume huyu hujamsikia akikwamakwama wakati anapoongea lakini ghafla unamskia akigugumiza anapoongea na wewe. Hii ni ishara ya kuonyesha kuwa anaishiwa na maneno ya kukuambia na inakuwa vigumu kwake kuyatoa ama kutafuta maneno ya kukuambia.

Je ni kitu gani kinachowafanya wanaume aina hii kuwa spesho kwa mwanamke?
Kuna wanawake ambao wanapenda wanaume ambao ni wa aibu kwa kuwa hawana mambo mengi. Lakini usishangae kumwona mwanaume wa aina hii akikuapproach akutoe mkale bata pamoja. Pia aina hii ya wanaume itafikia wakati fulani wanaweza kukushangaza kwa kufunguka na kugundua kuwa ilikuwa tu ni baadhi ya mbinu waliyotumia kukuteka kimapenzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *