Vitu Vinavyoweza Kuwa Sumu Katika Mapenzi.

Ni vizuri zaidi kuhisi kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana sana na kila mmoja amefika kwa mwenzie na hakuna kinachoweza kuwatenganisha, akini kumbuka kuna vitu unaweza kuvifanya katika mahusiano na ukahisi kuwa ni sehemu ya kumuonyesha ulienae kuwa unampenda lakini kumbe unaenda kubomoa kabisa huko mbeleni.Jaribu kuepuka vitu hivi ili kuhakikisha kuwa uliyenae anakuwa wako na anakupenda kadri siku zinavyoongezeka.

1.Usiwe na wivu kupindukia.

sio mbaya kuwa na wivu na mpenzi wako lakini kwanini ufanye wivu utakao mfanya hasiwe huru na mabo yake,kuna watu wanakuwa na wasiwasi na watu wao kwa sababu tu wanaongea na watu wnegine au wanakuwa karibu na watu wasio wajua.hii inamfanya mpenzi wako haisi kuwa haumwamini kabisa wakati kitu kikubwa kinachilinda uhusiano wenu ni kuaminiana.

2.Kutompa mpenzi wako nafasi.

sio mbaya kutaka kuwa na mpenzi wako karibu mud mwingi lakini kwanini ufanye asiw huru na mud wke. kuna muda atahitaji kuwa na marafiki zake au kufanya mambo yake binafsi, basi mpe nafasi. mfanye awe huru na kuwa na privacy yake, hata kama mna-spend muda mwingi pamoja kila mtu pia atenge muda wake na marafiki , ndugu au vitu binafsi.

3.Kumuingilia mpenzi wako katika mambo yake.

Kuna muda utatamani kumuambia mpenzi wako avae nini, akutane na nani, au afanye nini na wapi.Haikatazwi lakini jaribu kumzuia vitu ambavyo unaona vinakuwa na hatari ya kuhatarisha mapenzi yenu na hata kama unataka kumwambia sio ufanye kwa kulazimisha kumuambia aache hiki au kile.Ongea nae taratibu na mueleze kwaini hataki kam unaona anashindwa kuelewa nenda nae taratibu.Acha tabia ya kulazimisha na kuingilia mabo mengine unayoona hayana umuhimu kwako ukahisi hayana kwake pia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *