Mambo ya kuzingatia wakati wa kuchagua mchumba

Hamna raha ya pekee kama kuwa kwenye mahusiano ambayo mume na mke au ‘boyfriend’ na ‘girlfriend’ wanaelewana vizuri. Ni vigumu kupata mtu ambaye mnaelewana kila jambo.

Sio lazima kama mwenzako anasapoti Arsenal na wewe usapoti Arsenal. Wataalamu wa masuala ya mahusiano wanashauri kuwa, ili uweze kuishi vizuri na mtu kama mume na mke ni vizuri kuwa mnaelewana kwenye masuala ya msingi na mnashea visheni moja ya maisha.

Kati ya masuala ya msingi ambayo ni muhimu kuwa kwenye ukurasa mmoja ni Matumizi ya fedha na kujamiiana. Haya ndio mambo makuu mawili ambayo yanasababisha ndoa nyingi sana kuvunjika.

 Utajuaje matumizi ya mtu ya fedha kama ndio wachumba na bado hamjaanza kuishi pamoja? 
Ni rahisi, utakuwa unajua mwenzako anafanya kazi wapi, dadisi kwa watu kuwa kazi kama anayofanya mwenzako ina mshahara kiasi gani pamoja na dili nyingine anazofanya, ukishajua hilo anza kuchunguza matumizi yake, vitu anavyonunua, mavazi anayovaa, gari analoendesha na mambo mengine kama hayo. Kama matumizi yake yako juu kuliko kipato chake, jaribu kuongea naye na kumshauri kuhusu matumizi yake.

Tunakuja kwenye swala ya kujamiiana, hili ndio jambo la pili ambalo linaongoza kwa kusababisha mahusiano kuvunjika hasa kwa kizazi kipya. Miaka kama 30 iliyopita, watu wengi walikuwa wanaoana wakiwa bado bikra. Jambo zuri la kuoana mkiwa bado bikra ni kwamba wote mnaingia mkiwa hamna ujuzi na hamna wasichana au wanaume wengine ambao umelala nao wa kulinganishe ujuzi wao na mke wako au mume wako. Tatizo lipo siku hizi ambapo watu wanaoana wakiwa na ujuzi tofauti (diffetent experience level) ndio maana michepuko imezidi.

Wanadamu tumezoea kulingalisha vitu, pale utakapoanza tu kulinganisha utaalamu wa mwenzako na wanawake au wanaume wako wa zamani ndio utakapoanza kumuona mwenzako hafai. Jitahidi kutolinganisha uhusiano wako na watu waliopita, hamna watu wawili wanafanana kila kitu humu duniani. Kabla sijamalizia, napenda kusisitizia kuhusu umuhimu wa mawasiliano, sio kupigiana simu na kuandikiana message kwenye whatsapp, kutaneni mahali, wekeni simu zenu mbali na sio unaangalia picha instagram wakati unaongea na mwenzako.

Tafuteni sehemu iliyotulia mara mbili kwa wiki mzungumze na kupanga maisha yenu, usiogope wala kuona haya kuuliza swali lolote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *